KUNDI la watu wanaodhanikiwa kuwa ni majambazi wenye mapanga, marungu na nondo wamevamia Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa Yombo Kuu na kumjeruhi vibaya mlinzi wa kanisa hilo.
Mmoja wa walinzi wa kanisa hilo Richard Lameck ambaye alikuwa na mjeruhiwa aliliambia wa andishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa majambazi hao walivamia kanisa hilo saa 8:30 usiku wa kuamkia jana.
Alisema majambazi wanane walifanikiwa kuingia ndani ya kanisa hilo kwa kuruka ukuta na kisha kumjeruhi mwenzake huyo kwa kutumia nondo na hivyo kumsababisha majeraha kichwani na mkononi yalisababisha avuje damu nyingi.
Hata hivyo alisema kulikuwa na kila dalili ya kuwepo majambazi wengine nje ambao walikuwa wakisikilizia kinachoendelea kwa wenzao walioingia.
Lameck alifafanua kuwa tofauti na mambazi wengine hawa baada ya kuingia walikuwa wakielekea moja kwa moja katika eneo la madhabahu ambapo hata mwenzake huyo alijeruhiwa akiwa ndani ya kanisa hilo linaloendelea kujengwa.
Akizungumizia tukio hilo Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Joshua Jaha alisema haamini moja kwa moja kama watu hao ni majambazi kwa kuwa wangeiba mali ya kanisa hilo badala yake waliekea madhabahuni.
Alisema hata hivyo hawajui eneo hilo wangeenda kufanya nini kwa kuwa hawakuweza kulifikia baada ya mlinzi Lameck kufanikiwa kwenda eneo ilipo kengele na kugonja na hivyo kuwaogopesha na kuwafanya watimue mbio.
Alisema kutokana na tukio kama hilo kutokea katika kanisa lao lililoko Mbahgala wiki iliyopita anafikiri kuwa lina sura ya udini.
Alifafanua kuwa alipigiwa siku usio huo na kufika kanisa hapo saa 11 alfajiri ambapo alikuta damu zimetapakaa ndani ya kanisa hilo huku mlinzi alinusurika akimweleza kuwa zimtoka baada ya mwenzake kujeruhiwa.
Alisema alikimbizwa katika Hospitali ya Amani ambapo alishonwa nyuzi nne eneo la kichwani na tiba katika mkono ambao nao alijeruhiwa.
Alifafanua kuwa hali ya majeruhi inaendelea vizuri.
Ametoa mwito kwa viongozi wa makanisa kuimarisha ulinzi hasa katika wakati huu ambapo kuna matishio lakini kikubwa kingine wadumu katika maombi.