HISTORY
Zingiwa ni neno linalotokana na jina la mtu na tukio lilotokea.Mtu huyo jina lake alikua Zingi
Mzee Zingi alikua ni mmoja mkazi wa pwani katika wilaya ya kisarawe miaka mingi iliyopita, Mzee huyo ndiye babu wa kina siliyamungu. huyo mzee alikua na mke wake ambaye alikua akifanya shughulisha na sanaa ya ufinyangaji vyungu na mituni.
Inasemakana mzee huyo alikua ana safiri kutoka pwani kwenda mvuti akitumia njia ya kibelu kupitia bonde la nyasui, siku moja mzee huyo katika safari hiyo mzee huyo alikua ameambatana na mke wake, walipofika katikati la bonde hilo mkewe alitamani sana udongo wa maeneo hayo ambao udongo wake uklukua nzuri kwa shuhuri za ufinyanga
Mwanamke huyo alimushawishi mumewe wahamie pale ili waishi kwa shughuri ya kilimo na ufinyanzi, kwa hilo walihamia hapo kwa muda mrefu sana na badae, historia inaonyesha kuwa siku moja ilinyesha mvua usiku, na bahada ya mvuwa hiyo kunyesha maji yarifurika kidede, cha manyani, kitomondo ambao ndiyo uliyo ungana na mto lubarali mpakani mwa kitanga na nzasa.
Mafuriko hayo yalisababisha mzee zingi na mkewe wote walipotee kwa kuzama na maji na kuazinia siku, hadi leo pale paliko kua panachimbwa udongo inatengeneza chem chemi na palifikia mnyama kiboko aishi pale na kwa utamaduni wetu kizazi kilibadili kilikuwa kina kwenda kufanya matambiko hivyo ikapelekea hata wavuvi walipotaka kuvua lazima wamtafute mtu wa familia ya kina sili ya munngu. kutokana na tukio hilo watu wengi walishangazwa na kusema kwa mzee Zingi kuna nziwa na baadae kwa utamaduni wetu wa kili mmoja kuwa na mtani wa kina Siliyamungu nao wakaibuka na kuwa tani kuwa mzee zingiziwa kugeuka ziwa ndiyo mpaka sasa panaitwa zingiziwa yani mzee Zingi kageuka ziwa- kwa kifupi ZINGI ZIWA
Kutokana ziwa hilo ilipofika 15/10/1998 aliyekua makamo wa rais Dk. Omari Al Juma alipiga marufuku shughuri za kibinadamu ili kukilinda chanzo hicho cha maji na ilipofika mwaka 2000 hadi 2001, halimashauri ya manisipa ya Ilala iliamua kuanzisha hifadhi ndogo ya wanyama poli yani (zoo) kwa malengo ya sehemu ya utali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, Shule za misingi na sekondari pia na kupatiya vijana ajira